Rayvanny na Mpenzi Wake Wasemekana Kuachana
Mwanamuziki wa Bongo fleva kutoka katika label ya WCB Rayvanny na mpenzi wake Fahima ambaye pia ni mama wa mtoto wao mmoja Jayden, wamerudi katika vichwa vya habari baada ya tetesi kusambaa mtandaoni kuwa wameachana ambapo chanzo ni mchepuko.
Rayvanny na Fahima wamekuwa wakitawala vichwa vya habari katika siku za hivi karibuni na tetesi za wawili hao kuachana lakini mara kwa mara imekuwa mara tu baada ya habari hizo kuenea wawili hao wanaonekana tena pamoja.
Sakata hilo lilianza baada ya Rayvanny kupitia ukurasa wake wa Instagram kuweka ujumbe huu wenye utata ambapo aliandika;
Mpende ila usimuamini, Mpe ila sio vyote mtunze ila usimchunge, mpe mwili wako ila usimpe siri zako Ata mkojo ulikuwa soda mwanzoni, utamu ndio vichungu, Keep it in your mind”.
Baada ya Rayvanny kuweka ujumbe huo uliibua maswali mengi kwenye vichwa vya watu kuhusu nini hasa alimaanisha kwa maneno yale au endapo alikuwa anampiga kijembe mpenzi wake. Lakini Fahima naye alijibu mapigo kwa kuweka picha hii;
Ambapo chini ya picha hiyo ilisindikizwa namaneno ‘Single mama’ yenye kumaanisha hana mpenzi anamlea mtoto wake mwenyewe.
Miezi michache iliyopita tukio kama hili lilitokea baada ya picha ya Rayvanny akiwa na msichana mwingine wakiwa katika pozi lenye utata kusambaa mtandaoni na Fahima kutishia kumuacha lakini waliendelea na mapenzi kama kawaida. Wapendanao hawa wanajulikana kwa kupenda kurushiana vijembe kwenye mitandao ya kijamii lakini mwishoni hubaki pamoja na kulea mtoto wao.
Lakini mpaka sasa sio Rayvanny wala Fahima aliyeweka wazi kuwa wameachana au badoo wako pamoja.