Msaga Sumu Awatahadhalisha Wanawake Wanaomshobokea.
Msanii kinara wa muziki wa singeli nchini Selemani Jabiri maarufu kama Msaga Sumu amefungukia swala la tabia za wanawake wanaokuwa wakisumbua wasanii katika mitandao ya kijamii na hata kutafuta namba zao za simu kwa ajili ya kuwataka kimapenzi bila kujua kuwa wasanii wengine wanafamila zao tayari.Msaga Sumu anawahasa wanaokuwa wanamsumbua na wanamtaka kimapenzi kuwa yeye ana mke na watoto wawili hivyo anawaomba wamuache kabisa kwa sababu anaipenda familia yake.
Msaga Sumu ambae alipata kujulikana zaidi na wimbo wake wa mwanaume mashine amesemakuwa amekuw akisumbuliwa sana na wanawake kimapenzi lakini anachowashangaa ni kwamba wapo wanaojua kuwa yeye anafamilia yenye mke na watoto hivyo anaomba sana kutokusumbuliwa sana.
Imekuwa kero sasa , ninachoweza kuwaambia tu ni kwamba wanawake waache kabisa kunishobokea shobokea kwanza watambue kuwa nina familia lakini pia wajue kuwa ninaipenda sana familia yangu na ninatimiza miaka nane ya ndoa yangu kwa sasa. Na nina watoto wawili Inshallah Mungu kanijalia. Alifunguka Msaga Sumu
Hata hivyo msanii huyo wa singeli akiendelea kuongelea swala lake la muziki anasema kuwa kwa sasa ameshajipanga na anakaribia kuzindua mwanaume mashine .
kwa sasa najipanga kuzindua mwanaume mashine ndani ya dar live soon ntatangaza kuwajulisha kuhusu hilo. Alimalizia Msaga Sumu
Wasanii wengi wamekuwa wakilalamika hasa wa kiume kuwa wamekuwa wakifatwa dm kuuliza kuhusu maisha yao ya kimahusiano na hata wanawake wengine kuwataka kimapenzi , ukiachana na Msaga Sumu wasanii wengi wa kiume wamekuwa wakifungukia swala la wanawake kuwataka kimapenzi hivyo wanaomba kupunguziwa shuruba hizo kwa sababu wengine wana familia.