Shamsa Ford Ampa Darasa La Ndoa Shiloleh
Mwanadada mrembo anaejihususha na bongo movies lakini pia ni mjasiriamali maarufu baada ya kuijingiza huko baada ya kuolewa na mpenzi wake Chid Mapenzi, amefunguka na kumsahuri mwanadada Zuwena maaarufu kama Shiloleh jina la kisanii juu ya maisha ya ndoa aliyoyaanza hivi karibuni.
Shiloleh amefunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu kidogo anaejuliakana kwa jian la Uchebe wiki iliyopita ndoa ambayo ili-trend sana katika mitandao baada ya kuwashangaza watu wengi amabo walihisi kuwa ndoa hiyo haitaweza kufungwa kutokana na migogoro iliyojitokeza hivi karibuni baada ya kuvuja picha zikimuonyesha mwanadada huyo akiwa na mpenzi wake wa zamani ambae pia ni msanii mwenzie Nuh Mziwanda .
Shamsa Ford akitumia uzoefu wa ndioa yake aliyofunga mapema mwaka huu amemshauri Shiloleh kutulia katika ndoa yake na kuachana na sifa za kuwa maarufu kutokana na usanii wake bali atulie ili kuweza kufaidi matunda ya ndoa yake.
Katika ukurasa wake wa instagram Shamsa ameamua kufunguka kuhusu swala ilo na kumpongeza kwa uamuzi aliouchukua
Hongera sana mama umefanya maamuzi sahihi ya kumpendeza Mwenyezi Mungu cha muhimi uwe mke bora wa kitanzania kwa mumeo na ustar uache pembeni ‘mumuweke Mungu mbele yenu,uvumulivu na kuheshimiana Inshallah mtazikana,karibu kwenye chama mama …sasa nyie mnaosubiri matajiri wawaoe wakati matajiri wana wake zao mtasubiri sana mpaka uso uote sugu,uzuri na ustar uana mwisho wake itafika muda hata inzi hakusogelei. HONGERA MAMA
Alichokiandika shamsa ford katika ukurasa wake wa instagram
Mwisho huu w mwaka umekuwa mwaka mzuri kwa baadhi ya wasanii ambao wameamua kuachana na ukapela na kujiingiza katika maswala ya familia.PONGEZI NYINGI KWA SHILOLEH NA MUME WAKE.