Dogo Janja Amefunguka Jinsi Mke Wake Irene Uwoya Alivyobadili Maisha Yake

Mwanamuziki wa Bongo fleva Abdul Chande jina la usanii Dogo Janja amefunguka kwa mara ya kwanza na kueleza jinsi mke wake Irene Uwoya alivyo yabadilisha maisha yake.

Nina uthubutu wa kusema kuwa ndoa ya mwaka na ndoa iliyotikisa kila kona ya mwaka 2017 ilikuwa ni ndoa ya muigizaji wa Bongo movie na Irene Uwoya na Dogo Janja iliyofungwa mwezi uliopita.

download latest music    

Ndoa hii ilizua guzo kubwa sana hasa kwa sababu tofauti kubwa ya kiumei iliyopo baina yao lakini pia tofauti ya hadhi au kipato hasa wait walikuwa wakiangalia wanamuona Irene kama msichana mrembo sana hivo kuwa na uhusiano na kijana mdogo kama Dogo Janja ni kitu ambacho walikuwa hawakiamini.

Lakini mwezi na wiki kadhaa zimepita sasa na kila mtu taratibu ameielewa ndoa yao na Dogo Janja kwenye mahojiano aliyofanya na East Africa Tv kwenye kipindi cha Planet Bongo, amefunguka na kueleza kuwa anampenda sana make wake lakini pia amebadilisha sana maisha yake tangu amuoe.

Kwa sasa Ndoa yao bado ni changa mno lakini Dogo Janja amekiri na kusema kuna mambo mengi ambayo yamebadilika kwenye maisha yake kwa ajili ya muongozo wa mke wake kwenye maisha yake. Pia Dogo Janja amekiri kuwa uwepo Wa Krish kwenye Maisha yake kumemsaidia kutaka kuwa mtu bora zaidi ili awe mfano kwake.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.