Afande Sele Alia Na Mpoto,Ni Kuhusu Christian Bella na Uzalendo.
Msanii mkongwe wa muziki tanzania ambae kwa sasa anaonekana kupumzika kufanya kazi hiyo maeibuka juzi na kumvaa msanii mwenzie mkongwe pia , Mrisho Mpoto kuhusu wimbo wa uzalendo ambao uliimbwa siku ya kumbukumbu ya uhuru wa Tanzania ambapo wasanii wa kizazi kipya wali-perfom wimbo wa uzalendo wa nchi katika viwanja vya jamhuri mjiji Dodoma.
Hata hivyo Afande Sele anamlamikia Mpoto kwa madai kuwa alitoa baadhi ya wasanii na kumuweka Christian Bella ambae sio mtanzania na kuacha wasanii wa kitanzania na kumwambia kitu hicho sio uzalendo hata kidogo.
Rafiki yangu Mpoto kama kweli wewe ndie uliekuwa kinara katika katika utayarishaji wa wimbo maalum wa kuhamasisha uzalendo kwa taifa na bado ukaweza kushawishi kuondolewa kwa baadhi ya wasanii wazawa na kuweza kumpa nafasi hiyo rafiki yetu Christian Bella kushiriki katika wimbo huo unaowahusu watanzania ilihali unajua fika kuwa rafikiyetu bella ni kweli kuwa ni rafiki yetu lakini sio mtanzania bali ni mcongoman.
Kwa mujibu wa Afande Sele anaona kuwa Christian Bella hana haki ya kuimba wimbo huo kutokana na uraia wake na kwamba waliondolewa katika wimbo huo walipaswa kupewa nafasi kubwa kuliko yeye.
Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamemjia juu mwanamuziki Afande Sele na kumwambia kuwa pamoja na kwamba Bella ni mkongo lakini bado anafanya vizuri katika kukuza muziki wa Tanzania kwaio huo pia ni uzalendo na kama angejijua kuwa hastaili kuimba wimbo wa uzalendo wa taifa lingine angekataa lakini kwa sababu ya uzalendo ndio maana alikubali kuimba.