Baada Ya Kurudi CCM Wema Amaliza Bifu Lake na RC. Paul Makonda
Muigizaji maarufu wa Bongo movie Wema Sepetu amezidi kuzua gumzo mtandaoni baada ya wikiendi hiikurusha picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam, Paul Makonda.
Mwezi februari mwaka huu Wema pamoja na wasanii wenzake mbali mbali Kama Rachel Kizunguzungu, T.I.D, Rommy Jones, Petit Man Wakuache na wengineo walikamatwa na kuwekwa ndani wakituhumiwa kwa kujihusisha na matumizi na kuuza madawa ya kulevya.
Wengi wa wasanii hao waliachiwa wakaenda huru lakini Wema alifunguliwa kesi mahakamani baada ya polisi kuthibitisha kuwa walienda kupiga sachi nyumba yake na kumkuta na mihadarati kama misokoto ya bangi, kutokana na kesi hiyo Wema alihama CCM na kuhamia Chadema. Baada ya kesi hiyo Wema alianzisha bifu zito na Mkuu wa mkoa Paul Makonda.
Watu wengi waliamini kitendo cha Wema Sepetu kutajwa na RC Makonda kwenye orodha ya wasanii wanaotuhumiwa kujihusisha na madawa ya kulevya kulimaliza urafiki waliokuwa nao.
Jana kupitia ukurasa wake Istagram Wema aliwashangaza watu wengi baada ya kurusha picha akiwa amepiga pozi na RC. Makonda aliyo aliambatanisha na maneno haya:
With Le brother….Me Commander….The man himself I call him Mr. Dar es Salaam tupo all smile happy Sunday to you all kila lenye mwanzo lazima liwe na mwisho”.
Kwa njia hiyo Wema ameamua kuwaonyesha mashabiki zake kuwa hayo yote yameisha na kwa sasa amerudi CCM na amerudisha urafiki na Makonda kama ilivyokuwa zamani.