Snura Asema Faiza Ally Anatafuta Pa Kutokea
Baada ya kugombana kwa muda mrefu na kutupiana maneno katika mitandao ya kijaamii baada ya msanii Faiza Ally kuweka picha yake iliyoonesha utupu wake akiwa leba kipindi anajifungua mtoto wa pili amabapo watu wengi ikiwepo wasanii kukwazika na kitendo cha mwanadada huyo kudharirisha wanawake wenzie na ndipo Snura alipoamua kumtolea uvivu na kumwambia ukweli.
Hata hivyo baada ya Snura kumwambia ukweli ilileta tafrani kwa sababu Faiza aliona kitu alichokifanya yuko sawa kabisa tofauti na vile watu walivyochukulia.
Mwanadada Snura amefunguka tena na kusema kuwa alichokifanya mwanadada huyo ni kosa la kimaadili kwa jamii sema kuzuka kwa ugomvi wao ni sawa na kutafuta kiki kwa dada huyo kwa sababu nyimbo ambazo yeye anaimba haziweka maungo ya mwili wa mwanamke uchi kama alivyofanya yeye hivyo mwanadada huyo anatafuta pa kutokea tu.
Akiongea na Risasi, Snura anasema kuwa kwanza nyimbo zake hazihamamsishi ngono kama yeye anavyosema lakini pia pamoja na kwamba mwanadada huyo amemtukana mitandaoni lakini ujumbe aliompa atakuwa ameshajifunza hata kama hataki kukubali kuwa amejifunza.
Ninachojua huyo anatafuta pa kutokea tu , maana mimi nyimbo zangu hazimaanishi ngono hata kidogo hizo ni fikra zake na siwezi kumzua hata kidogo , mimi ninachokijua ni kwamba nyimbo zangu zinaonyesha uhalisia wa watanzania kama zilivyo ngoma zetu.
Hata hivyo picha hiyo ambayo ilizua tafrani katika mitandao iliwezz kufutwa dakika chache na wamiliki wa mtandao wa instagram baaada ya kuripotiwa na watu kuwa haukuwa inaendana na maadili ya kitanzania.
Kwa Faiza Ally kuweka picha za aina hii ni jambo la kawaida kwake , hii sio mara ya kwanza na haitakuwa mara ya mwisho kutokana na kauli zake anazowajibu watu wanaomshauri kutokufanya kitu hicho.