Baada Ya Babu Seya na Papii Kocha Kuachiwa Huru Hili Ndio Jambo La Kwanza Walifanya

Siku ya Jumamosi 9 Desemba ilikuwa ni siku kubwa ya kihistoria sio tu kwa sababu ilikuwa ni siku ya kusheherekea miaka 56 ya Uhuru wa Tanzania bali pia Watanzania walipata kitu kingine cha kuwapa furaha baada ya Babu Seya na mwanaye Papii Kocha kuachiwa huru kwa msamaha wa raisi.

Juni 25, 2004, Hakimu mkuu mkazi wa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, Addy Lyamuya aliwahukumu aliwahukumu kifungo cha maisha gerezani Babu Seya au Nguza Viking na Papii Kocha katika gereza la Ukonga baada ya kukutwa na hatia ya kubaka na kunajisi watoto kumi.

download latest music    

Siku ya Uhuru 9 Desemba, Raisi Wa Jamhuri ya Muungano John Pombe Magufuli alitangaza katika hotuba yake alipokuwa anawahutubia wananchi kuwa ameamua kuwasamehe:

Kutokana na hiyo hiyo Ibara ya  45 kuwasamehe familia ya Nguza Viking jina jingine anaitwa Babu Seya pamoja na ndugu Johnson Nguza au kwa jina jingine pia ni Papii Kocha hivyo nao waachiwe huru kuanzia Leo”.

Baada ya Raisi kutangaza habari hizo ukumbi mzima ulilipuka kwa shangwe na vifijo lakini pia kwenye mitandao ya kijamii watu wote walifurahi na wananchi kwa ujumla waligubikwa kwa furaha.

Jioni ile baada ya kutangazwa kusamehewa Babu Seya na Papii Kocha waliachiwa huru kutoka katika gereza la Ukonga ambapo walipokelewa na nyomi la wananchi waliowazingira kila kona huku waandishi wa habari wakiwapiga picha.

Lakini mara tu walipopata Uhuru Babu Seya na Papii Kocha walielekea katika kanisa la Life Christian (Zoe) walipoenda kuonana na Mchungaji kwa ajili ya kupata maombi baada ya ombi Lao la kutoka jela kujibiwa.

 

 

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.