Banana: Mambo Ya Familia Yasichanganywe na Usanii
Banana ni moja ya wasanii wakongwe toka kuanza kuimba kama kundi katika familia mpaka sasa kuwa na bendi yake mwenyewe.Akielezea historia ya familia yake utakuja kujua kuwa pamoja na kuwa na kipaji cha kuimba na kazi anayoifanya kwa ujumla lakini pia familia ilikuwa ina mchango mkubwa sana kwa banana zoro kuweza kufanikiwa kufanya kazi zake za muziki.
Banana alianza kuimba akiwa katika bendi ya baba yake mzazi akiwa na dada yake Maunda Zoro ambapo baba yao ndio alikuwa akiwalea kimuziki na mpaka alipokuka kuanza kuimba mwenyewe na sasa kuwa ni moja ya wasanii wakongwe wanaomiliki bendi na kuajiri watu wengine pia.
Lakini historia yake haimfungi yeye kuwafanya watoto wake na familia yake haswa watoto wake kushindwa kujiamulia kile wanataka kufanya na kuwa katika maisha.Pamoja na kwamba hata wao wanaweza kuwa na vipaji lakini hataki kuwa na nguvu ya kuwaambia nini familia yake hasa watoto wafanye kwa sababu na yeye alifanya.
Banana Zoro anasema kuwa unapokuwa katika familia basi inabidi mambo yakae kifamilia na sio kuchanganya mambo ya familia na usanii.watoto katika familia wanapaswa kuachwa kuchangua nini wanataka kufanya na kuacha ustaaa mbele.
Umaarufu ni gharama sana, nawaacha watoto wangu wachague wnyewe ni kitu gani nwanataka kufanya , lazima wachague kati ya umaarufu na maisha yao ya kawaida ya baadae ila kitu kikubwa ni lazima tuwaelekeze katika elimu.
Hata hivyo Banana Zoro anasema kuwa watu hawapaswi kuwa na mambo mengi na ni lazima kujua kuwa sio vizuri kuchangantya maisha yako ya familia na yale mambo ya kuwa staa.
Unapochanganya usanii na familia unaweza kuharibu kila kitu na mfumo mzima wa familia ,usichanganye vitu hivi viwili.
Banana amekuwa msanii wa muda mrefu huku akitamba na nyimbo kama nzela, mama yangu na Mapenzi gani.