Gigy Money Awaamkia Wanaotangaza Kuwa Ana Mimba
ingawa mimba huwa ni jambo la kheri lakini inakuwa tofauti kwa baadhi ya wasichana hasa wasanii wa tasnia za sanii nchini, wengi wamekuwa wakikana kuwa na mimba au hata kama wanazo baadae tutaona zinayeyuka na kushindwa kujitetea wapi imekwenda.Kutunza mimba na kutoa mtoto mwenye afya njema na mipango ya Mungu lakini pale inapogundulika kuwa uma mimba swala linalofuata ni kushukuru Mungu na kutulia.
Hivi karibuni msanii gigy money aliweka picha katika mtandao wa instagram ambayo ilionyesha tumbo lake kuwa kubwa na watu kuanza kusema kuwa inawezekana gigy money atakuwa na mimba kutokana na picha hiyo lakini pia kutokana na maneno aliyokuwa ameandika katika posti ile.Hata hivyo Gigy Money aliwajibu baadhi ya mashabiki walihisi kuwa ana mimba na kuwakanushia taarifa hizo.
Akiongea na Star Mix ya GPL ,Gigy Money ambae alikuwa akionekana kweli ameanza kunawiri na kitumbo chake kuanza kuonekana kama mtu mwenye ujauzito amesema kuwa watu waache kumuandama. Gigy money anasema kuwa yeye kuwa na mimba au kutokuwa na mimba haimuhsu mtu na hata kama ana mimba sio lazima kutangaza na kila mtu kujua swala hilo.
Kama nina mimba au sina mimba haimuhusu mtu, kwa sababu mimba sio kitu cha matangazona kama ninayo tu mtajua kwa maana mimba haifichiki kabisa, kuhusu mwili wangu kuanza kuongezeka ni kweli mara ya kwanza nilikuwa nina stress sana sasa hivi niko poa sana ndio maana nimeanza kunenepa.
Gigy money ambae sasa hivi yupo kwenye mahaba mazito na mtangazaji mwenzie anaejulikana kama DJ Mo inasemekana kuwa kweli walnategemea mtoto ingawa Gigy Money mwenyewe anakanusha taaarifa hizo.
Gigy Money na mpenzi wake