Mama Diamond Athibitisha Kuolewa
Mama wa msanii mkubwa wa bongo fleva nchini na nje ya nchi Diamond platinumz anaejulikana kama BiSandra amethibitisha kufunga ndoa hivi karibuni.Mama huyo anasema kuwa kwa muda mrefu walikuwa wakisema amekuwa akionekana na mwanaume akitoka nae na kusemekana kuwa ni mpenzi wake basi ni kweli kuwa mwanaume huyo ni kweli ndie aliemuoa kwa sasa.
Akionesha hadi pete ya ndoa kidoleni kwake , mama huyo anasema kuwa ni kweli ameolewa na wanaosema kuwa mwanaume huyo ni mdogo kwake wamuache kwa sababu angekuwa mdogo asingeweza kuoa , lakini kwa sababu umri wake unaruhusu ndio maana ameweza kuoa.
Nimeolewa na mwanaume yule yule ambae walikuwa wanamsema katika mitandao kwa sababu ndio nilimpenda,wanaosema mdogo anaudogo gani angekuwa mdodgo asingeweza kunioa.
Hata hivyo mama huyo anasema kuwa kwa sasa watu wategemee kuona mdogo wake na Diamond anakaribia kuja,kwa sababu watu wanataka mdogo basi na yeye atamuongezea Naseeb mdogo wake wa mwisho.
Akiongelea posti ambazo amekuwa akizituma huku zingine zikiwa zinasheheni mambo ya ugomvi na umbea umbea mama huyo amesema kuwa anaamua kuweka posti hizo ili kuweza kusisimua watu wanaomfuata waweze kuendelea kumfuata na kuongea mashabiki kwa sababu ustaa ndio unawafanya wao kufanya hivyo.