Linah:Huwezi Kubadili Dini Kwa Sababu Ya Mapenzi
Mwanadada aliyekuwa anafanya vizuri katika muziki wa kizazi kwa mud mrefu nyuma ambae kipaji chake kilitengenezw a vizuri kutoka THT , jumba kubwa lenye vipaji Linah Sanga amefunguka kuwa ni vigumu kwa mtu kubadili dini kwa sababu ya mapenzi na inawezekana ni kweli kuwa dini imekuwa ni kikwazo kwa watu wengi kushindwa kufanikisha ndoto hiyo.
Hata hivyo mwanadada huyo ambae yuko kwenye mahusiano na mwanaume ambae wanatofautiana dini huku Linah mwenyewe akijulikana kuwa ametoka katika familia ambayo wanaamini sana dini kwa upande wa kikristo alishawahi kusema kuwa hata kama mwanaume huyo aliebahatika nae kupata mtoto mmoja wana dini tofauti haimaanishi kuwa watashindwa kuishi pamoja.
Mwanadada huyo anasema kuwa swala la kubadili dini iwe ni sababu ya imani yako kukutuma kufanya hivyo lakini sio kubadilisha dini kwa sababu ya kufata mapenzi kwa mtu fulani.
Unajua kiimani utakiwi kufanya vitu juu juu,na hata kama unataka kubadilisha dini basi iwe ni kwa sababu ya dini na imani yako lakini sio kwa sababu ya mapenzi hata siku moja, kwaiyo mimi sikutaka kufanya iyo michezo ila ninaamini kuwa patalegea tu popote pale au tutfunga ndoa hivyohivyo na Mungu mwenyewe atalegeza kwa sababu tunapendana na tayari tuna mtoto anaetuunganisha kwa hilo.-Alifunguka Linah
Hata hivyo katika kuongezea swala hilo Linah alisema kuwa kwa upande wa familia ,familia zote zimekuwa ni ngumu kukubaliana kwa sababu pande zote zimejidhatiti katika dini yao,
Kwetu nahisi ndio sana japo kwao kwao pia ni wagumu lakini nahisi ni kotte kote tu maana kwao ni waislamu sana na sisi ni wakristo sana.