Kemmy Amtia Moyo Lulu Michael, Awapa Pole Wazazi.
Mwana mama mkongwe kutoka katika tasnia ya filamu nchini Kemmy amefunguka na kuongelea mchango alikuwnao Dr.Cheni katika kumtoa Lulu katika tasnia ya filamu lakini pia ameonyesha kuguswa kwake na matatizo aliyoyapata na kuwapa pole watu wa karibu na Lulu.Mama huyo ameonysha kuguswa kwake kutokana na kile kilichompata Lulu cha kufungwa kifungo cha miaka miwili jeal baada ya kukutwa na hatia ya kuua bila kukusudia.
Kemmy anasema kuwa anatambua kuwa Dr.Cheni ndie aligundua kipaji chake na kwamba kwa mara ya kwanza alipokuwa na miaka saba na anaijua safari yake ya maisha hasa katika sanaa.Kemyy anasema kuwa wao ni watu wa kwanza kumjua na kujua kipaji cha lulu na kwamba hata anayopitia ni mapito katika maisha.
Kemmy anamwambia Lulu kuwa mateso anayoyapata sasa ni kwa sababu za tamaa za watu wachache waliomuona na kutaka kumuangamiza .
Uchungu wa mwana aujuaye mzazi,hata kama sio kubeba tumboni,lakini baada ya dr.cheni kugundua alikuleta kaole ukiwa kama na miaka saba,naifahamu kwa sehemu safari yako, Mungu anakupenda na ndio maana anataka upitie haya.Maisha hayana uzoefu na hakuna anaejua safari yake.
Wale waliokutesa na kukuumiza kwa tamaa zao ,ndio waliokupa wakati mgumu unaopitia sasa lakini Mungu akukumbuke na kukufutia hatia ya damu ambayo haukukusudia kuimwaga.kama mtoto mikononi mwa mikono ya mtu mzima aliyelewa,amejaa hasira na ghadhabu na kipigo na kama mama ninajua kitu gani ulikuwa unapitia, ulikuwa katika hali ya kujitetea na uhai wako na ndio hayo yote yakatokea.
Lakini usiogope na Mungu ni mwaminifu sana, na huruma nyingi si mwepesi wa hasira Isaya 1..18,dhambi nyekundu kama damu uzifanya nyeupe kama theluji,Mungu akukumbuke na akusamehe ili upate nafasi ya kuwasamehe pia wale waliokuumiza, na ukitoka kwenye hilo darasa ukawe na mwanzo mpya.Nakuombea maisha marefu ili unapotoka ukaanze maisha mapya yenye ushindi , hapo utakuwa hukushindwa bali umeshinda zaidi ya kushinda, Mungu akawe nguzo yako na msaada tela kwa wakati huu mgumu.NAKUPENDA BINTI YANGU,MUNGU AKULINDE.