Sasha Aelezea Alivyoteswa Na Kifo Cha Ndikumana.
Mmoja wa wauza nyago nchin katika video za wasanii mbalimbali anaejulikana kama Sasha Kassim amefunguka na kusema kuwa alipokea kwa uzuni sana habari za kifo cha mchezaji wa mpira Hamad Ndikumana kwa sababu katika watu aliokuwa akiwapenda tangu zamani ilikuwa ni kuwaona irene uwoya akiwa na mwanasoka huyo.
Sasha anasema kuwa alikuwa akivutiwa sana anaposoma taarifa za wawili hao na kusema kuwa kwake ilikuwa ni couple bora sana kuliko couple zozote Tanzania na ndio maana aliumia sana kusikia Ndikumana amefariki Dunia.
mwanadada huyo anaendelea kusema kuwa kwa muda wote wa msiba huo hakuwa na mood ya kufanya kitu chochote kile zaidi ya kukaa ndani kwa huzuni aliyokuwa nayo baada ya kupata taarifa hizo.
Katika couple ambayo nilikuwa nikiipenda sana ni kati ya Ndikumana na Irene Uwoya tangu kipindi nasoma.Nilikuwa napenda kuwasoma na kuwafatilia katika magazeti sana , na kwakweli kifo cha Ndikumana kimeniumiza sana sana. Alifunguka mwanadada huyo ambae alionekana kuwa na huzuni.
Marehemu Ndikumna enzi za uhai wake akiwa na mtoto wake aliyezaa na Uwoya
Ndikumana alifariki Dunia wiki chache zilizopita mwezi huu na kuzikwa huko kwao Rwanda ambapo alifariki kwa matatizo ya ugonjwa wa moyo kwa ghafla .Hata hivyo kifo hicho kilizua gumzo na kusemekana kuwa ugonjwa wa mwanasoka huyo ulisababishwa na mawazo ya muda mrefu kutokana n akumuwaza mkewe Urene uwoya alieolewa hivi juzi juzi na msanii wa bongo fleva.
Irene alipata bahati ya kutembelea kaburi la mwanasoka huyo akiambatana na familia yake yaani mama yake na mtoto wao wa kiume mpaka rwanda ambapo alipokelewa vizuri na familia ya Ndikumana tofauti na vile watu walivyofikiria kuwa angeweza kukataliwa na ndugu wa marehemu.Ndugu wa Ddikumana akiwepo baba yake walimpa baraka zote Irene Uwoya na kumuombea mazuri.