Masogange Amuepusha Mwanae Na Vita Vya Mitandaoni
Wasanii wengi wamekuwa wakitukanwa katika mitandao ya kijamii na mashabiki zao au maadui zao wanapofanya jambo fulani ambalo linaweza kuwa baya kwa baadhi ya watu na likaonekana zuri kwa baadhi ya watu.Na hata wanapoanza kutukana au kukufatilia watu wanakuwa hawajali wale watu waliopo nyuma yako na inawezekana kabisa hata watu wa karibu yako wakaweza kuathirika na vita hizo kutoka kwa mashabiki au mahasimu wako.
Wasanii wamekuwa wakivumilia mengi kutoka kwa mashabiki zao, wengi wamekuwa wakiona ndugu zao , watu wa karibu na hata wanafamilia kutukanwa na kuingizwa katika mambo ambayo ilipaswa kuwaathiri wasanii wenyewe kwa sababu ndio wanaofanya hadharani.
Agness Masogange amefunguka na kuongelea swala ilo na kukiri kuwa hata iweje hawezi kumuweka mtoto wake katika mitandao kwa sababu ameshajua watu wengi wakiaanza kuku-attack wataingiza hadi watu wako wa karibu, Agness ambae ana mtoto wa kike mwenye miaka nane amesema kuwa kama mtoto wake atataka kujiigiza kwenye mitandao atajiingiza akishakuwa lakini sio kwa sasa akiwa mdogo kwa sababu watu wanapokuwa wanatukana hawajali kuwa yule ni mtoto.
Siwezi kumnadi mwanangu hiyo ni misingi yangu niliyojiwekea kabisa,kama atapenda mambo ya kwenye mitandao atakuja kujiingiza yeye mwenyewe lakini sio mimi maana watu nawajua. Alifunguka agness masogange.
Muuza nyago huyo alipata umaarufu mkubwa wa jina la Masogange baada ya kutokea katika video ya Belle 9 ya Masogange
Haya yote yanakuja baada ya muda mfupi uliopita ambapo mwanadada huyu pia alikuwa akilalalmika jinsi watu katika kitandao wamekuwa wakimsema vibaya na kumsingizia baadhi ya mambo ambayo hayana ukweli ndani yake.Mwanadada huyo kwa sasa anakabiliwa na kesi ya matumizi ya madawa ya kulevya na kesi yake mekuwa ikisomwa katika mahakama ya Kisutu.