Wema Atoa Siri Ya Kupungua Kwa Mwili Wake.
Watu wamekuwa wakishangaa na wengine wakisema vibaya pale wanapoona mtu fulani amekonda kwa ghafa, alianza Gigy Money ambae watu walisema sana kuhusu kukonda kwake na baadae Gigy Money alikuja kusema kuwa alikuwa akifanya diet na kunywa dawa za kupunguza uzito.
Hivi karibuni baadhi ya mashabiki wa msanii Wema Sepetu walianza kuongea katika mitandao kuhusu kupungua kwa mwili wa mpenzi wao wema sepetu na kuwa ameanza kukonda na kuisha kabisa huku kila mmoja akitoa sababu zake tofauti huku zingine zikienda katika upande wa afya yake.
Akiongea na gazeti la ijumaa wema sepetu amewajibu mashabiki wake na kusema kuwa sio kweli kuhusu watu wanavyosema vibaya kuhusu afya yake bali ameamua kupunguza mwili wake kwa sababu amona kuwa unaongezeka kila kukicha bila kuwa na staa ya kuvaa baadhi ya nguo.
Unajua nilikuwa nikiangalia kila nguo ninayovaa inanibana.wakati mwingine unakuta nguo ni kubwa kabisa lakini hainotoshi kabisa.nikaona nina kila sababu ya kupunguza mwili wangu ambao sio hata mzuri hata kwa afya-Alisema Wema sepetu.
Muonekano wa Wema Sepetu wa sasa
Hivi karibuni Wema Sepetu alikuwa nchini Rwanda ambapo alikwenda katika instagram party ambapo alikutana na mashabiki na watu wake wanaomfuatra katika mtandao wa instagram.