Matukio ya Fiesta Dar,Mamia Wakesha Mpaka Asubuhi
Ikiwa ndio kilele cha Fiesta mkoani Dar Es Salaam kimefanyika wikiendi hii ya tarehe 25, huku ikiwa na vikwazo vya muda na vitu vya hapa na pale, tamasha hilo limeweza kufanikiwa kuisha kwa kishindo kikubwa huku ukumbi wa Leaders ukiwa umefurika.watu wengi kama ilivyotegemewa wamefika katika tamsha hilo na kuonekana kulifurahia huku wakimshukuru raisi wa Tanzani aliyewaruhusu watanzania kustareheka katika tamasha hilo mpaka saa kumi na mbili asubuhi.
Mashabiki wa muziki na watu mbalimbali wakiwa katika msafara kuingia ukumbini.
Baadhi ya wasanii wakiingia ukumbini tayari kwa ajili ya kufanya show ya tigo fiesta.
Kushoto ni Ben pol na Vannesa Mdee, kulia ni Ben Pol,Jux na Barnaba katika picha ya pamoja wakisubiri kutoa burudani kwa mashabiki
kundi a Weusi katika picha ya pamoja na mtangazaji wa Clouds Media, Shadee
Nandy katika muonekano wa tofauti kidogo akisubiri kukutana na mashabiki wake.
Chin Beez akiwa jukwaani .
Vannesa Mdee nae akifanya yake akiwa na madancers wake, kivazi chake pia kilileta gumzo.
Ben Pol akiwa na Tausi , huyu ni moja ya wasanii wanaotajwa kuwa wabunifu sana katika kila mkoa aliobahatika kufanya show,Ben Pol amekuwa akijitahidi sana kuleta sura mpya.
kushoto Alikiba alipokuwa jukwaani, kulia Alikiba na Ommy Dimpozi kwa pamoja.
Maua Sama akiwa jukwaani.