Mama Mzazi Wa Wema Akutana Na Cha Moto Mahakamani
Ikiwa leo ni tarehe ya kusikilizwa kwa kesi ya Wema Sepetu ambayo bado ilikuwa kwenye muendelezo , na huku Wema Sepetu akionekana katika mitandao ya kijamii akiwa nje ya nchi alipokwenda kwa ajili ya special appearance katika instagram party nchini humu, mama mzazi wa Wema Sepetu alikwenda mahakama kwa ajili ya kutoa hudhuru ya mwanadada huyo.
Katika kesi iyo wakili wa serikalai Augustino Michael aliitaja kesi iyo mbele ya hakimu Simba na kusema kuwa ndio ilipaswa kushughulikiwa kwa muda huo lakini kitu cha ajabu mama mzazi wa Wema Sepetu alinyoosha mkono na kuomba kupatiwa nafasi kuwa alikuwa ana jambo anataka kulisema.
Baada ya kunyoosha , hakimu alimpa nafasi mama huyo na mama huyo alisema kuwa Wema Sepetu amepata hudhuru na kushindwa kuhudhuria katika kesi hiyo huku akisema kuwa alikuwa amepata msiba wa kufiwa na shangazi yake.
Mheshimiwa Wema amepatwa na hudhuru ya kufiwa na shangazi yake kwaio amekwenda kushghulikia swala la mazishi, ndio maana ameshindwa kuhudhuria mahakamani hapa leo, na mimi mama yake nimekuja kumuwakilisha.
Hakimu anaeshughulikia kesi hiyo alipomaliza kusikiliza hudhuru hiyo alimuuliza mama huyo kama Wema amepata msiba na kushindwa kufika mahakamani imekuwaje yeye mama yake ameweza kupata muda wa kufika hapo.
Hakimu alimuonya mama yake Wema na kumwambia kuwa siku nyingine hapaswi kufanyia mchezo swala kama hilo la kutokufika mahakamani hapo. Kesi hiyo imehairishwa mpaka tarehe 14 December mwaka huu.
Wema anakabiriwa na kesi ya kukutwa na kutumia madawa ya kulevya.
Hata hivyo taarifa za kutokufika mahakamani kwa Wema zimekuwa hazina ukweli wowote kwa sababu msanii huyo amekuwa akionekana akipost katika ukurasa wake wa Instagram kuwa yupo nchi ya jirani kwa ajili ya kukutana na mashabiki wake na watu wa nchi hiyo ambao wanatumia mtandao wa instagram.