Kifo Cha Ndikumana Chazidi Kuzua Utata, Ndoa Ya Dogo Janja na Uwoya Yahusishwa

Siku mbili zilizopita Hamad Ndikumana Kataut alifariki dunia, Ndikumana alipata umaarufu nchini baada ya kumuoa muigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya na kizaa naye mtoto mmoja wa kiume.

Ndikumana alifariki ghafla siku mbili zilizopita bila kuumwa ugonjwa wowote ingawa watu wengi wanadhani kuwa alipata ugonjwa wa moyo lakini lakini kiukweli ugonjwa kamili uliomuua haujawekwa wazi.

download latest music    

Watu wake wa karibu wamedai kuwa siku ambayo alifariki alihudhuria mazoezi na timu yake ya Mpira aliyokuwa anacheza za Rayon sports, ambapo ofisa habari wa Rayon Sports Oliver Gwakaya amedai kuwa

Alisikia maumivu makali kwenye kifua akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza tu kunywa kidogo akatapika na akaishiwa pumzi”.

Kwenye mahojiano aliyoyafanya na gazeti la Amani, Haruni Niyonzima ambaye alikuwa rafiki wa karibu wa Ndikumana alisema marehemu alilalamika maumivu ya kifua mara baada ya kumaliza mazoezi alirudi nyumbani na kutafuta daktari bila mafanikio ndipo alipowahishwa hospitali ambapo mauti ilimkuta:

Nimepokea kwa masikitiko Kifo cha Ndikumana nimeongea na watu wa kule nyumbani (Rwanda) wanasema alishiriki vizuri mazoezi, mara baada ya mazoezi kumalizika alilalamika maumivu ya kifua akarudi nyumbani ambapo maumivu yalizidi baadae kukimbizwa hospitali ambapo mauti ilimkuta”.

Hizi siku chache kabla ya kufariki Ndikumana alitumia sana mitandao ya kijamii kuonyesha hisia zake za kuumia baada ya mkewe Uwoya kuolewa na Dogo Janja ambapo alilalamika mara kwa mara. Watu wote wa karibu na Ndikumana wameweka wazi kuwa kitendo cha kuachwa na Irene kilimuumiza Sana kwa muda mrefu lakini aliumia zaidi pale alijia kuwa Irene ameolewa, kuna wadau wamedai kuwa ugonjwa wa moyo ulimpata Kisa penzi la Irene hasa pale alipoolewa na Dogo Janja.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.