Mwenye Jina La Tatoo Ya Uwoya Akana Kumjua Mrembo Huyo
Kulikuwa na tetesi kuwa moja ya vijana matajiri Tanzania anaejulikana kwa jina la Salaah alikuwa na uhusiano wa mapenzi na msanii Irene Uwoya, lakini tetesi hizo zilikanushwa na kijana huyo baada ya kuulizwa kuhusu habari hizo.
Kipindi cha nyuma kidogo Irene Uwoya alionekana akijinadi na tatoo kubwa mgongoni kwake iliyokuwa imechorwa jina la Salaah, na ikathibisha kuwa mpaka mrembo huyo kuweza kumchora tatoo hiyo basi ni kweli kuwa wawili hao watakuwa na uhusiano wa kimapenzi lakini tetesi hizo zilikuja kuzimwa baada ya mwanadada Irene Uwoya kuolewa na msani mwenzie Dogo Janja.
Muonekano wa tatoo ya yenye jina la kijana mmoja tajiri mgongoni mwa Uwoya.
Moja ya watu wa karibu wa Irene aliwahi kuthibitisha na kusema kuwa jamaa huyo alikuwa amekufa na kuoza kwa mrembo Irene na kutokana na upendo huu mwanadada aliamua kumuonyesha kwa kumchora tatoo hiyo ya jina lake mgongoni.
Hata hivyo moja ya magazeti pendwa kutoka Global walitaka kumtafuta Irene Uwoya , hii ilikuwa kabla hajapata matatizo ya msiba lakini juhudi hizo hazikuzaa matunda, lakini waandishi hao hawakutaka kuishia hapo ndipo walipoamua kuanza kutafuta namba za kijana huyo tajiri nchini ili kuulizia kuhusu tetesi hizo.
kijana huyo alipatikana kwa njia ya simu lakini alisema kuwa yuko nje ya nchi hiyo hawezi kuonana nao lakini walipata nafasi ya kumuuliza papo kw apapo kuhusu tetesi hizo na kijana huyo alisema kuwa hana lolote analolijua kuhusu msichana huyo na kuhusu tatoo yeye hausiki na chochote.
Sikilza hayo mambo unayozungumzia mimi siyajui kabisa, wala huyo unaemtaja mimi simjui kabisa na ndo kwanza nakusikia wewe hapo unamsema , kwaio tafadhali kabisa naomba msiniusishe na hayo mambo. -Aliongea kijana huyo katika simu
Inakuwa kazi kwa baadhi ya watu wanaojikuta wakichora tatoo za kudumu katika miili yao na kushindwa kufutika kwa sababu wanapoachana na wapenzi hao alama hizo zinabaki katika miili yao.
Irene Uwoya kwa sasa yupo katika kipindi kigumu kutokana na kufiwa na mwanaume aliefunga nae ndo kanisani na mzazi mwenzie Hamad Ndikumana Kataut.