Bendi Ya Msondo Ngoma Yawaburuza WCB Mahakamani na Kutaka Fidia ya Milioni 300

Bendi kongwe katika mziki wa dansi nchini Msondo Ngoma Music Band, wameiburuza mahakamani  label ya Wasafi Classic inayoongozwa na mkali wa Bongo fleva Diamond Platnumz.

Habari hizo zilitapatakaa mtandaoni Jana kwa kile kinachodaiwa na Msondo kuwa kikundi cha wasanii kutoka Wasafi kilichowajumuisha Diamond, Rich Mavoko, Lava Lava, Queen Darleen, Mbosso, Harmonize na Rayvanny walitoa wimbo wao unaoitwa Zilipendwa lakini waliiga melodi za Msondo Ngoma bila ruhusa yoyote.

download latest music    

Kwenye barua hiyo wakili wa bendi hiyo ya Msondo Ngoma iliwapa taarifa label hiyo kuwa wasanii wao walitoa nyimbo yao tarehe 25 agosti mwaka 2017 na kuuzwa dunia nzima katika vyanzo vyao mbalimbali na katika wimbo huo unaoitwa ‘Zilipendwa’ dakika ya 4:55 mpaka 5:10 walitumia mlio wa saksafoni na melodi zinazochukuliwa kwenye wimbo wa Msondo Ngoma ujulikanao kama ‘Ajari’ kwenye dakika ya 6:38 mpaka 6:52.

 

Barua hiyo iliwatahadharisha WCB kuwa kitendo chao cha kutumia kazi iliyobuniwa na kutungwa na Msondo Ngoma bila makubaliano nao ya kuwalipa chochote ni kosa kisheria kwani wamekiuka sheria za hatimiliki huku wakijua wazi kuwa wanavunja sheria.

Pia mawakili hao wamewakumbusha kuwa wanatambua kuwa tangu ‘zilipendwa’ imetoka wasanii hao wametengeneza hela nyingi sana kupitia wimbo huo lakini hawatambua mchango wa kisanaa wa ile melodi ya saksafoni waliotumia hivyo imewaomba label Hiyo ya ifidie kiasi cha shilingi milioni 300 ndani ya siku saba zijazo basi itawafikisha mahakamani mara moja.

 

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.