Barakah The Prince Kuwashtaki Rockstar 4000
Msanii wa Bongo fleva Barakah the Prince ameshika tena headline baada ya kuweka wazi nia yake ya dhati ya kumshtaki Boss wake wa zamani Seven Mosha pamoja na label nzima ya Rockstar 4000.
Barakah ameingia matatizoni na uongozi wake wa zamani, Rockstar 4000 na kumshutumu aliyekuwa boss wake. Baada ya kujitoa label hiyo ya Rockstar Barakah alitoa wimbo wake mpya unaojulikana kama ‘sometimes’ lakini tangu wimbo huo ameweka wimbo huo kwenye mtandao wa YouTube, Barakah amedai kuwa uongozi wake wa zamani umekuwa ukimfanyia vituko ilimradi asifanikiwe ambapo alisema walikuwa wanaifungia nyimbo hiyo ili nashabiki kutoka nchi za nje wasiiangalie.
Alipohojiwa na kituo cha televisheni cha East Africa, Barakah aliongelea ishu hiyo na kuweka wazi hatua za kisheria atakazochukua:
Nilijaribu kutengeneza YouTube account mpya ili niachane na ile ya mwanzo kwa sababu ilikuwa na matatizo na Rockstar walikuwa wanaing’ang’ania lakini baada tu ya kuweka video yangu mpya mayo ikaanza matatizo kama ile video ya mwanzoni viewers wanashuka badala ya kupanda kwaiyo hapa kuna watu wawili wanaoweza kufanya hivyo aidha ni watu wa Mxcarter au Seven kutoka Rockstar, na siwezi nikaongelea tena hili suala kwa sababu kesi ilishafunguliwa polisi tunasubiria kwenda mahakamani”.
Barakah alikosa maelewano na label hiyo ya Rockstar iliyokuwa inasimamia kazi sake za kimuziki baada ya kuamua kujitoa kwa kile alichodai walikuwa wanafanya uzembe na kazi zake hata hivyo Barakah amewasihi mashabiki zake wasikate tamaa kwani ataachia nyimbo nyingine hivi karibuni.