Banana Zorro Amejibu Tuhuma za Kufeli Kimuziki na Kufulia
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Banana Zahir Zorro amejibu tuhuma zinazomkabili za kuwa amefulia na pia muziki wake umekufa.
Banana anayetokea kwenye familia ya kimuziki ambapo baba yake Mzee Zahir Zorro na Dada yake Maunda Zorro, alitamba miaka ya nyuma kwa vibao kama ‘mama yangu’ ‘rafiki’ ‘ Zoba’ na vinginevyo vingi amekuwa kimya kwa kipindi kirefu tofauti na umaarufu aliokuwa nao kipindi cha nyuma, ingawa yeye mwenyewe amedai kuwa anafanya muziki na bendi yake ya The B- Band.
Kwenye mahojiano na kituo cha televisheni cha East Africa, Banana alifunguka yafuatayo kuhusiana na Tuhuma hizo:
Unajua mafanikio ni wewe ni dream yako ukiwa unakua huwezi ukasema sijafanikiwa kwasababu hunijui alafu isitoshe siwezi kuonyesha kila kitu nilichokuwa nacho lakini mimi Niko vizuri pia mimi ndio mwanamuziki pekee mwenyr bendi Tanzania nimeajiri wait zaidi ya ishirini mimi naona hayo ni mafanikio makubwa sana, kilichobaki hapa napambana nijulikane kimataifa tu lakini mziki wangu bado upo na bendi yangu tunapiga kila siku na watu wanalipa kuja kutuona kwaiyi mimi naona sijafulia”.
Lakini pia Banana amesisitiza kuwa anashangaa hizo tuhuma za yeye kukosa fedha zinatokea wapi kwani ana magari na pia ana nyumba yake aliyojenga mwenyewe tofauti na wasanii wengine wakongwe ambao amedai ndio wana hali mbaya.