Dogo Janja: Nilisota Sana Mpaka Kumpata Uwoya, Haikuwa Kazi Rahisi
Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Abdul Chande maarufu kama Dogo Janja amefunguka mambo mazito siri juu ya uhusiano wake mkewe mpya Irene au Sheila Uwoya.
Wiki hii nzima Dogo Janja na Uwoya wameshika vichwa vya habari kwa wingi baada ya kufunga ndoa wiki iloyopita siku ya Ijumaa, huku wengi wakikataa kuamini kuwa mtoto mdogo kama Dogo Janja anaweza kumpata mtoto mzuri kama Uwoya, leo kwenye mahojiano aliyofanya na clouds Fm katika kipindi cha Leo tena Dogo Janja amefunguka yafuatayo kuhusiana na mkewe Uwoya na ndoa yao kwa ujumla:
Kwanza kabisa hakuna kitu kinanisikitisha kama watu kuifananisha ndoa yangu na mimi kutafuta kiki na ndio maana tulifanya haya mambo kwa siri kubwa, kwa sababu sikutaka haya mambo yawe hivi kwani na mimi inaniumiza sana ninachotaka watu wajue kuwa nimeoa kweli , alafu isitoshe familia yangu imetoa baraka zote kwasababu kwanza kabisa nilishawahi kumpeleka Uwoya nyumbani na kusema ukweli mama alimfurahia sana na walicheka sana na nikamwambia mama basi mi nampenda sana huyu mwanamke na ntamuoa ili uendelee kufurahi zaidi kwaiyo nina baraka zote za mama yangu”.
Pia Dogo Janja amefunguka zaidi kuhusu uhusiano wake;
Unajua watu wengi wanaona kama mimi sistahili kuwa na Irene labda kutokana ni watu wawili tofauti lakini mimi Irene nimeanza kumpenda tangu zamani yaani nilikuwa nikimuangalia navutiwa naye yaani nimeamini kuwa ndoto huja kutokea kweli kitu kikubwa ni kuthubutu na kuvaa ujasiri yaani mpaka nampata Irene nimesota sana yaani haikuwa kazi rahisi mara ya kwanza alikuwa hataki hata kuniona lakini kutokana na nilimpenda nilivumilia mpaka leo hii tumefunga ndoa”.
Dogo Janja amesema ndoto yake siku moja wawili hao wawe na familia kwani anaamini Uwoya atakuja kuwa mama bora kwa familia yao.