Siwema :Kuachana Na Nay Kulinifunza Maisha

Mwanadada Siwema ambae ni mzazi mwenzie na Ney wa mitego amefunguka na kusema kuwa kitendo cha yeye kuachana na mpenzi wake huyo  kimemfanya aweze kujifunza na maisha na kusimama tena kuliko kukaa kubweteka na kuanza kulilia mpenzi kama wadada wengine wanavyokaa na kubweteka na mapenzi.

Siwema na Ney wa mitego walikuwa wapenzi kwa muda mrefu nyuma na kufikia hatua ya kupata mtoto mmoja lakini baadae walikuja kuachana baada ya kuwa na skendo nyingi za mwanadada huyo kuwa anatoka na vigogo wengi, hata hivyo tetesi zilikuwa zikisema kuwa kwa kipindi hicho ambacho dada huyo akiwa na mapenzi na Ney wa mitego alikuwa akitembea na wanaume wengine ili kupata ela kwa ajili ya kumpa mpenzi wake huyo ambae alikuwa bado hajakaa sawa kimuziki kwa miaka hiyo ya nyuma.

download latest music    

Hata hivyo mwanadada huyo alipitia mapito mengi mpaja kusweka rumande na kuachishwa kazi aliyokuwa akifanya kutokana na kuwa na scandal nyingi na wizi wa mali za ofisi.

Siwema anasema kuwa kama angekuwa amebweteka kipindi kilae alichopata matatizo na Ney na kukosa kazi hasingekuwa hapa alipo lakini anashukuru Mungu kwa sababu ana duka kubwa la nguo lililopo jijini Mwanza ambalo ndilo linamsdaidia kuendelesha maisha yake kwa sasa

“Unajua ukikumbwa na misukosuko tena hasa hii ya kimapenzi akili inatanuka sana kwa haraka sana, leo hii mimi nina duka langu kubwa la nguo  hapa jijini Mwanza  na maisha yangu yanaendele kama kawaida, sasa kama ningekaa kulilia penzi la Ney wa mitego ningechemka sana”

Hata baada ya kufanikiwa kupata mtoto pamoja bado lakini wawili hao walipogombana Ney wa mitego aliamua kumchukua mtoto wake huyo wa kiume na kumpeleka kwa bibi yake (mama yake mzazi na Ney)

 

About this writer:

Expedicto Lilian

#Godseeker, I am what i ought to be and always i will be, but am not what i used to be.