Mambo Atayoyafanya Nikki Wa Pili Akiwa Raisi
Mwanamuziki Nikki wa pili kutoka katika kundi la Weusi, ambalo linaundwa na wasanii watatu Joh Makini, G-Nako na Nikki wa Pili ,amefunguka na kuendelea kuonyesha nia yake ya kutaka kuingia kwenye siasa kwa spidi ya ajabu,Nikki wa Pili ambae anafanya vizuri wa kibao chake cha kihasara na quality time ambazo zinafanya vizuri zaidi katika vituo mbalimbali vya habari.
Nikki wa pili ametaja baadhi ya mambo muhimu atakayoyafanya endapo atakuwa raisi.Mwanamuziki huyo ambae alishawahi kusema kuwa anampango wa kuingia kwenye siasa anaendelea kuthibtisha nia yake hiyo kupitia maneno yake.Katika vitu alivyoviorodhesha ni pamoja na :
1.Kikao kikubwa cha serikali yangu itakuwa sio baraza la mawaziri bali mkutano mkuu wa kijiji au mtaa(kitaa kitaongea)
2.Kipimo kikubwa cha maendeleo itakuwa ni kupanda au kushuka kwa maisha ya watu sio vipimo vya kukua kwa uchumi au makusanyo ya fedha.
3.Mfumo wa elimu utajikita katika kupima learning na sio ufeli au kufaulu
4.Vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa vikifanya mikutano na kuhoji serikali sio vyama vya siasa bali vyama vya wakulima, wafanyakazi ,walimu, machinga , bodaboda madaktari na kadhalika.
5.Serikali itakuwa mdau mkubwa uchumi na mukewezaji atakuwa ni mkulima,mfugaji, mchimbaji mdogo,wavuvi wadogo na wafanyabiashara wadogo.
6,Ardhi, maji ,elimu ,afya, havitakuwa bidhaa bali hifadhi za jamii
7.Maisha bila maadili hayana maana , kila mtoto ni lazima afundishwe kuwa na maadili , uaminifu,heshima,ujamii,upendo, bidii, na kujiamini.
8,Mahusiano na mataifa ya afrika hayatakuwa na neno wahamiaji haramu , mwafrika hawezi kuwa haramu maana Afrika ni nyumbani kwake.
Nikki anasema kuwa maswali ataulizwa kipindi cha kampeni kikifika lakini anampango wa kuwa mgombea binafsi.
Nikki akiwa kama moja ya wasanii wenye ushawishi mkubwa na impact kubwa kwa jamii, atakapojiingiza katika siasa atakuwa amevumbua na kusaidia vijana wengine wengi wanaompenda na kumuamini pia.
Ukiachana na kazi za muziki anazofanya Nikki na wenzake lakini pia msanii huyu amekuwa akitumiwa na mashirika katika mikutano mbalimbali ya uhamasishaji wa vijana katika jamii.