Shusho Aongelea Ishu Yake Na Mashabiki Wake Wa Kenya
Yeye ni mmoja wa wanamama wanaopendwa sana na mashabiki zake hasa kwa sababu ya nyimbo zake za injili zinazosaidia kutia moyo na kutoa faraja, Christina Shusho ambae alijizolea mashabiki wengi zaidi nchini Kenya kuliko hata nchini Tanzania amefunguka na kuongelea ishu ya yeye kutukanwa na mashabiki wake wa nchini Kenya baada ya kupost picha ya moja wa wagombea wa uraisi nchini Kenya huku akiporomosha maombi kwa mgombea huyo.
Christina Shusho alipost picha ya Uhuru Kenyata na kutoa maombi kwake kwa kipindi hiki cha uchaguzi , lakini kitu cha kustaabisha ni kwamba mashabiki wake kutoka Kenya walimvaa kwa matusi katika ukurasa wake wa instagram na kumwambia kuwa anachofanya ni kuwagawa mashabiki wake.
Akiongea na East Africa Television , msanii Shusho anaelezea alivyoyapokea matusi hayo na alichukuliaje swala hilo na ni kitu gani aliamua kufanya ili kuwapoza mashabiki wake”unajua ile ni mihemuko tu inayokuwa iko miongoni mwa watu hasa katika kipindi kama hiki ambacho wakenya wanakipitia kwa sasa,mimi nilikuwa nafanya tu maombi nikasema sio shida nimuombee na raisi wa Kenya , basi wakanijia juu na kuanza kunitukana, wakawatafuta mpaka marafiki zangu wa kule wakaanza pia kuwatukana,ni kitendo ambacho kilinishtua sana nikaona basi isiwe tabu acha tu nimpost na huyo mwingine ili niweke usawa lakini naomba ndugu zangu wa kenya wajue kuwa sikuwa na nia yoyote ya kuwagawa au kuwa na upendeleo” alifunguka Christina Shusho
Christna Shusho ni mmoja wa wasanii wa kike wa injili wenye ushawishi mkubwa sana katika mitandao ya kijamii na ni kwa sababu amekuwa na mashabiki wengi sana, inawezekana ni kweli kuwa kitendo chake cha kupost mgombea wa upande mmoja kingefanya kupoteza baadhi ya mshabiki zake kwa sababu mashabiki wanaompenda ni watu wenye itikadi tofauti tofauti hivyo kufanya hivyo ni kuweka upendeleo kwa wale wanaomwamini mgombea huyo huko akionyesha kama kuwatenga wale wa upande mwingine, lakini pia alifanya vizuri alipoamua kuweka usawa katika hilo.
Nchi ya Kenya wanategemea kurudia kufanya uchaguzi wa uraisi tarehe 26 Oktoba.