Elimu ni Muhimu Kwa Wasanii Ili Kuondoa Ujinga- Ali Kiba
Mwanamuziki wa Bongo fleva, Ali Kiba ameongelea umuhimu wa elimu kwa wasanii.
Wasanii wengi wakishaingia kwenye sanaa yoyote wakapata njia ya kuingiza kipato wanaona hakuna umuhimu wa kusoma au kupata elimu ya darasani.
Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ali kiba aliongeza kuwa elimu inatoa ujinga na hivyo ni muhimu kwa wasanii wote kupata elimu.
Ukiwa na elimu kama wewe ni msanii ni rahisi kuonyesha watu ubongo wako ukoje, kwa sababu mkasa na visa vipo na maneno yapo lakini utamfanya mtu afikirie huyu mtu aliwaza nini, unajua ubongo wako ukiwa active utaweza kufikiria vitu vya msingi zaidi, achana na watu wanaoimba ujinga, ni kwasababu tu ya talent lakini elimu ni ya muhimu sana kwenye kila kitu”.
Ni kawaida kwa wasanii wengi kudai kuwa hawadhani kama kuna umuhimu wa kupata elimu ya darasani na hasa wakipata mafanikio lakini pia kuna wasanii wachache waliofanikiwa kupata elimu ya juu mfano wasanii kama Mwana Fa, Nikki Wa pili, Jokate na wengine wengi.
Je una maoni gani juu suala hili la elimu kwa wasanii, je unahisi kuna umuhimu wowote kwa wasanii kupata elimu?
Tafadhali toa maoni yako.