Kala Jeremiah Amuongelea Tundu Lissu
Mwanamuziki wa hip hop Kala Jeremiah amefunguka kuhusu kisa kilichotokea kwa mwanasiasa na mbunge wa Chadema Tundu Lissu.
Kala ambaye ni mmoja wa wasanii wa hip hop ambaye anapenda kuimba mambo ya siasa katika nyimbo zake kama Dear God, wimbo wa taifa na nyinginezo amesema unyama uliofanywa kwa Tundu Lissu umemshtua na kumshangaza kama ilivyokuwa kwa mtanzania yoyote.
Kala Jeremiah amefunguka;
“Kile kitendo alichofanyiwa Tundu Lissu lilinishtua ni tendo baya sana kwa nchi yetu kwa sababu hatujawahi kuzoea hivyo vitu unajua kuna nchi ambazo wakisikia jambo kama hilo wanaona kama kitu cha kawaida lakini kwetu lilishtua kila mtu aliye na akili timamu alishtushwa sana na habari hizo”.
Kala aliendelea kusema:
“Kile kitendo kinapeleka ujumbe mbaya kwa nchi nyingine kuhusiana na nchi yetu kwani kitu pekee ambacho nchi yetu inajivunia siku zote ni amani kwaiyo kitendo hicho kimeleta dosari sana, yapo matukio mengine lakini hilo ni tukio la kuhuzunisha sana”.
Kala Jeremiah aliyekuwa amekaa kimya kwa muda amerudi kwenye gemu na hivi sasa ana wimbo mpya unaoitwa ‘Kijana’.
Wasanii wengi wamekuwa waoga kuzungumzia siasa au hata matukio yanayotokea nchini Kama shambulizi la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu hasa ukizingatia msanii kama Roma alitekwa kutokana nakuongelea mambo yanayoendelea nchini, lakini wanaharakati kama Kala hutoa nyimbo za kuelimisha na kuhimiza mabadiliko katika jamii kwa hiyo Big up kwa Kala.