Prezo Ni Chawa Kama Chawa Wengine-Gigy Money
Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini anaefanya vizuri na kibao chake cha Nampa papa na video vixen anaefanya vizuri katika nyimbo za wasanii wengine na kutokea vizuri kabisa Gigy Money amefunguka na kutoa maneno ya kashfa kwa msanii wa muziki kutoka Kenya alikuja Tanzania hivi karibuni.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi na kusambaa kwa picha mitandaoni zinazomuonyesha msanii Prezo kutoka Kenya akiwa na mmoja wa msanii wa kike na video queen wa Bongo Amber Lulu, ambapo mashabiki waliongelea sana picha hizo,akiwa kama rafiki wa karibu wa msanii huyo , Gigy Money alifunguka na kumtetea rafiki yake kutokana na matusi ya mtandaoni aliyokuwa akitukanwa na mashabiki baada ya picha izo kusambaa.
Gigy Moneya aliongea maneno ya kashfa kidogo kuhusu msanii Prezo akisema kuwa watu wasishangae kuona Lulu anafatwa na Prezo Tanzania kwa kuwa na yeye pia ni kama wanaume wengine tu”Prezzo ni chawa tu kama chawa wengine tunaweka, we kamshobokea katoka kenya kuja mpaka huku Tanzania unashangaa nini,umemuona Lulu kaenda Kenya huko,mzuri huyo sio mbaya,kwaiyo nyie tulieni tu, na wengine watakuja kutoka Madagascar,Uk,” alifunguka Gigy Money alipokuwa akiongea na eNews ya EATV
Gigy Money na Amber Lulu ni marafiki wa muda mrefu wakianza kazi kwa kupiga picha na baadae kuwa video queens, lakini sasa wamefanya vizuri kwa kuonyesha vipaji vyao katika kuimba na wameoneka kukubalika katika soko la muziki ingawa wamekuwa ni moja wa wasanii wa kike wanaokubwa sana na scandal za wanaume ambazo kwa namna moja au nyingine zinaharibu kazi zao za muziki.