Faiza Ally: Sugu ni Mwanaume Ambaye Hajielewi Sina Muda Wa Kumnyenyekea
Mwanamitindo na muigizaji Faiza Ally amefunguka tena kuhusiana na uhusiano wake na baba wa mtoto wake wa kwanza Mh. Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ Mbunge wa Mbeya Mjini.
Faiza na Sugu wamekuwa katika mabishano ya muda mrefu sana kuhusiana na malezi ya mtoto wao huku Faiza amemshtaki Sugu kwa kukataa kutoa fedha za matunzo ya binti yao.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amefunguka yafuatayo;
“Kuna wanaume wapumbavu sana mimi nitapigana mwanangu atakua lakini kumbuka sina cha kupoteza mtoto atakapo kuwa wewe ndio utakua umepoteza muda wa kumtunza mwanao kwa sababu ya kuni punish mimi na ujinga wangu! Lakini mimi ntakua nimetimiza majukumu yangu kama mzazi na huenda matusi yangu ndio yananipunguzia stress kwa namna fulani ili maisha yaendelee….sasa weweendelea kunikomesha siku hazigandi”.
Pia Faiza aliendelea kufunguka kwa kulalamika kukerwa na kilichotokea baina yao;
“Ila tu ujue nikiwa najisikia ntakuchamba tu mpaka ntakapo choka na hata nikiacha ntakua nimeacha kwa sababu nimechoka lakini sio eti ni ache ndo umtunze mwanao, mtunze ndo niache kama humtunzi siachi nikijisikia nakupa za uso mpaka uelekee na usipo elekea basi lakini siwezi kukunyenyekea mpaka nakufa”.