Mashabiki Wanapendelea Zaidi Nyimbo Za Mapenzi-Lady JD
Mwanamuziki mkongwe wa Bongo fleva Lady Jay Dee amefunguka kuhusiana na sababu za yeye na wanamuziki wengi kupendelea zaidi kuimba nyimbo za mapenzi.
Lady Jay Dee amesema kuwa sio kweli anaimba sana mapenzi bali ni mashabiki zake ndio wanapenda.
Lady Jay Dee ambaye kwa sasa anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘I miss you’ amesema hayo kwenye mahojiano aliyoyafanya na kituo cha televisheni cha TBC ambapo alifunguka;
“Mashabiki wanasikiliza wanachokipenda zaidi kwa hiyo nafikiria ndio watu huwa wanapenda mapenzi siyo kwamba mimi ndio huwa naimba mapenzi sana”.
Pia katika mahojiano hayo Lady Jay Dee alifunguka kuhusu ongezeko kubwa la wasanii wa kike katika mziki wa Bongo fleva;
“Nafurahi sana kwa sababu kwa kipindi kirefu kumekuwa na uhaba wa wasanii wa kike na kila tunapoenda tunaulizwa kwa nini wanamuziki wa kike si wengi lakini kwa sasa kuna unafuu mabinti wameongezeka, wamejitokeza”.