Irene Uwoya Achoshwa na Maswali kuhusiana na Uhusiano Wake na Dogo Janja
Mwigizaji wa Bongo movie Irene Uwoya amefunguka kuwa amechoshwa na watu wanamuuliza kuhusiana na uhusiano wake na Mwanamuziki Dogo Janja.
Kumekuwa na tetesi nyingi kuwa Irene Uwoya na Dogo Janja wana uhusiano wa kimapenzi, uhusiano huu umekuwa ukileta gumzo kwenye mitandao ya kijamii kutokana na tofauti kubwa ya kiumri iliyopo baina yao. Dogo Janja ana umri wa miaka ishirini na mbili (22) na Mrembo Uwoya andaiwa kuwa na umri wa miaka ishirini na tisa (29), Huku bado kukiwa hamna uthibitisho Kama wawili hao ni wapenzi maneno hayo yamebaki kuwa ni tetesi tu.
Katika mahojiano aliyoyafanya na kipindi cha ‘over the weekend’ Irene alifunguka kuwa amechoshwa na kuulizwa maswali juu ya yeye kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Dogo Janja ni suala lake binafsi na hahitaji kuulizwa na haijalishi atakuwa na mtu anayemtaka.
“Sitaki na sihitaji kumzungumzia Dogo Janja na nimechoshwa na maswali kuhusu kuwa kwenye mahusiano naye hayo ni mambo yangu binafsi na ninaomba niachwe kwa kweli”.
Warembo wengi wa Bongo movie wanasifika kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na vijana wenye umri mdogo kuliko wao huku wakijulikana kwa majina kama Serengeti boys, ben-10.