Mahakama ya Kenya yasimamisha mkataba uliyobuniwa wa madaktari wa Tanzania kufanya kazi nchini humo
Mkataba uliyobuniwa kati ya serikali ya Kenya na Tanzania kupeleka madaktari nchini humo umesimamishwa na koti.
Madaktari wa Kenya walienda mahakamani kuizuia serikali ya nchi hiyo kutoa ajira hizo wakidai kuwa kuna madaktari 1,400 wasio na ajira nchini humo.
Wamelalamika kuwa itakuwa ni ufujaji wa fedha kuwa na madakrari 500 wa Kitanzania watakaolipwa tshs 360,000 kwa siku. Mahakama ya kazi imetoa agizo hilo Ijumaa jii (March 31), ikisema kuwa litadumu hadi ombi la maofisa wa afya litakaposikilizwa na kuchambuliwa.
That leave is hereby granted…to quash the decision of the government…to hire foreign doctors to be deployed to Kenya,” zimesema nyaraka za mahakama za March 31.