Harmonize azungumzia madai ya kwamba ana maringo
Mwanamuziki wa Wasafi Harmonize leo katika kipindi can East Afrika Mashariki, humo Kenya alizungumzia madai ya kwamba ana maringo mengi na hataki kuhusiana na watu.
Akiongea katika show ya Mzazi Willy Tuva, alieleza ya kwamba yeye hana marigo mbali ako busy tu na mambo yake. Alieleza ya kwamba label yake ya Wasafi imetengezea time table ambayo anaifuata kwa ukamilifu.
Kama hayuko ofisini akifanya muziki ako nyumbani kwenye gym ama chumbani mwake akilala. Yeye hana haja yoyote ya kutembelea vyumba vya viburudisho.