Sababu Za Aslay Kutoa Nyimbo Mpya Kila Siku
Ile tabia ya bandika bandua kwa Aslay haiwezi kukoma kwa kipindi hiki kwa sababu kadri watu wanavyozidi kusema kuhusu tabia ya baadhi ya wasnii kutoa nyimbo mpya kila siku ndo kwanza yeye anazidisha.Aslay ambae kwa sasa nafanya vizuri kabisa katika muziki na amekuwa akitoa nyimbo mfululizo na zote zinapokelewa vizuri na mashabiki wake.
Wiki iliyopita msanii huyu alitoa wimbo mwingine mpya alijulikan kama ‘natamba’, wimbo ambao baada tu ya kutoka ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya mashabiki kuonekana kuuelewa sana,wimbo huu.Hivyo Aslay amuamua kufunguka na kutoa sababu za ya yeye kutoa nyimbo mpya kila siku.
Akiongea na EA Radio katika kipindi cha Planet Bongo Aslay alisema kuwa kwa sasa inambidi atengeneze nyimbo zake mwenyewe ili aweze kuepukana na kuimba nyimbo za band katika show kwa sababu kwa sasa afanyi kazi na band”tangu nimetoka kwenye band nimekuwa nikifanya kazi peke yangu, nategemea show zangu na nyimbo zangu tu sio nyimbo za band tena,ndio maana nafanya kutoa nyimbo nyingi,ilimradi hata nikipata show niwe natumia nyimbo zangu” alisema Aslay
Ikimbukwe kuwa Aslay alikuwa katika kundi la Ya Moto Band lililokuwa likiundwa na vijana wanne lakini kundi ilo kwa sasa limevunjika na kila mtu anafanya kazi peke yake huku yeye Aslay akiwa chini ya meneja wake Chambuso na Maromboso ikisemekana kuwa amesajiliwa katika Lebel kubwa kabisa Tanzania ya Wcb, wengine bado wapo kimya.
Hata hivyo Aslay anaonekana kujiamini na kile kitu anafanya na anasema kuwa ni kwasababu kazi zake nzuri na zinapokelewa vizuri na mashabiki, neno ambalo sio mara ya kwanza kwa msanii huyu kulisema”kingine natoa kazi nyingi kwa sababu ni nzuri,kazi nzuri ikikaa ndani huwa naagopa kwa sababu naogopa idea ya kugongana , kazi nzuri ukitoa leo na nyingine ukatoa kesho watu watapenda tu kwa sababu ni nzuri” alimalizia Aslay.
Hivi karibuni msanii huyo ametoa nyimbo kama ‘mhudumu’, ‘pusha’,’likizo’ na ‘baby’ na zote zinafanya vizuri sokoni.