Ben Pol Amfananisha Msaga Sumu Na Dr.Remmy
Ni wasanii wachache sana wanaokubali kazi za wasanii wenzao tena hasa wanapokuja katika swala zima la kazi za musiki kwa sababu wengi wanaamini kuwa ili kufanikiwa kimuziki basi lazima kuwe na ushindani.Hii imekuwa tofauti kwa msanii wa Bongo Fleva anaejulikana kwa kufanya vizuri na kupewa jina la king of Rnb , msanii Ben Pol ambae ameibuka na kuusifia sna muziki wa msanii mwenzie Msaga Sumu.
Akiongea na kipindi kinachorushwa na Clouds Radio cha XXL, Ben Pol ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘kidume’ alichomshirikisha mwanadada mrembo kabisa kutoka Nigeria Chidinma Chikere, Ben Pol anasema anavutiwa sana na ufanyaji muziki wa msanii mwenzie Msaga Sumu.
Sijui kama Msaga Sumu ni upcoming artist au sio lakini napenda sana muziki wake na jinsi anavyokuja , ana-flavor , yake kama Dr.remmy au sound flani hivi ya kitofauti sana, na ninamuona jinsi atakavyofika mbali katika muziki wake’ alifunguka Ben Pol kuhusu Msaga Sumu
Ben Pol anaendelea kumuongelea Msaga Sumu na kusema kuwa ni msanii mwenye kipaji cha kuweza kubadilika badilika na kuimba nyimbo zenye radha tofauti tofauti”Alafu anaweza kubadilikabadilika kila mara, mara nyingine anaweza kuimba zilipendwa, au anaweza kuimba singeli, kama oya oya oya lakini ni msanii mwenye vitu vingi sana” aliongezea ben pol
Msaga Sumu ni mmoja wa wasanii wanaochipukia na kufanya vizuri katika game la muziki hasa katika style hii mpya ya muziki wa kisingeli iliyopo sokoni kwa sasa, hata hivyo Msaga Sumu anaweza kuita mwanzilishi wa kisingeli na ndiO msanii alijitaidi hata kuhamamsisha wasanii wengine wadogo kufanya muziki wa kisingeli hivyo kusababisha kukua kwa kisingeli.Msaga Sumu kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha singeli kinachojulikana kama “mwanaume mashine” inayopendwa sana hadi na watoto kutokana na style yake ya kuimba na kucheza huku ikitaja baadhi ya majina maarufu ya wacheza mpira na timu kubwa nchini , hapo mwanzo alifanya vizuri na kibao cha “unanitega shemeji’.