Idris Aomba Msamaha Kwa Hamisa Mobeto
Baada ya kujibizana katika mitandao mchekeshaji maarufu, mwanamitindo , mjasirimali na mtangazaji Idris Sultani pamoja na Video queen mashuhuli nchini Hamisa Mobeto, Idris aamua kuomba msamaha kama kile alichokiposti siku chache katika mtandao kimemkwaza mrembo huyo.
Mwezi huu tarehe 2 ilikuwa ni birthday ya msanii mkubwa nchini Diamond Platinumz na watu wengi walimpongeza msanii huyo katika kuazimisha siku yake hiyo, mmoja kati ya watu hao alikuwa ni Idris Sultani, lakini kama ilivyo kawaida ya Idris uweka zaidi utani mbele karibia kwa kila jambo analolifanya hivyo hata katika kumtakia siku nzuri Diamond aliamndika maneneo yenye utani ila kubwa zaidi ni pale aliposema anampa zawadi ya shilingi mia tano ili akanunue condom kwa ajili ya kupunguza matumizi kwa watoto wengi atakaowazaa na gharama za kununua rav 4.Ujumbe huu uliopokelewa vibaya na mwanadada Hamisa Mobeto ambae ni mzazi mwenzie na Diamond Platinumz ambae hivi karibuni tu walikuwa na vita kubwa baada ya Diamond kukataa mimba ya mwanadada huyo na hata baada ya kujifungua mtoto.
Baada ya post hiyo ya Idris, Hamisa nae aliamua kumtolea povu zito Idris akimwambia aachane na mambo hayo kwa sababau yalishapita na anaombwa kupumzishwa kwa maana alishasemwa sana na sasa imetosha.Lakini kwa kuwa Idrsi alifanya kama utani kwa Diamond anahisi hasingeweza kumkwaza mtu basi aliamua kuchukua jukumu la kuomba msamaha kwa post yake iyo.
“Heshima niliyonayo kwa kimama na wanawake wote ni kubwa sana tena hasa hasa kwakua nimelelewa na mama mwenye uvumilivu,mpiganaji,na wakuijua dini sana,jazba na huzuni wanazopitia wazazi ni kubwa sana hasa unapokuwa na mtoto wa miezi 9 bila kuweza kumshusha hata mara moja upumzike kidogo, unavimba miguu, unalia sana, unapata vichomi, unabadilika sura, unashindwa hata kutembea ,na unaanza kula vitu hata uelewi,.mwaka baada ya kujifungua kuna mengi katika kumfunza kutembea na kushika meza,kutaja maneno vichache na kula vyakula vigumu pia kutambua zuri na baya kwa kuona.As for that najua hakuna thamani ya pesa inaweza kuweka kutathmini yote anayopitia mama .With this i respect women to the extent that thamani wanayoweza kulipwa nayo ni kwa maisha au kumpa moyo wako kabisa .This is deep truth ,the rest tunafanya utani because we just want to make things easy and laugh, my apologies if I have offended any woman for this.Regards,Idris” aliandika idris katika ukurasa wake wa Instagram