Haya Ndio Maneno Ambayo Hamisa Mobetto Kamuandikia Mtoto Wake na Diamond

Mrembo Hamisa Mobetto ambaye ni mzazi mwenzie na msanii Diamond Platnumz ameweka wazi hisia zake dhidi ya mtoto wake Dylan ambaye amezaa na Diamond.

Tangu Diamond akubali kuzaa na Hamisa amekuwa katika vichwa vya habari mara kwa mara kukosolewa na watu wengi sana ni leo tu ametoka kumtetea mtoto wake dhidi ya utani wa mchekeshaji Idris Sultan.

download latest music    

Kwa kupitia ukurasa wake wa Instagram Hamisa ameandika maneno yafuatayo kwa ajili ya mtoto wake;

“Wewe ni mfalme wangu, wewe ni zaidi ya Kinga yangu, Wewe ni maisha yangu, Wewe ni zaidi ya Almasi, Wewe ni zaidi ya pesa kwangu, Navyokupenda ni Mungu tu ndo anajua”.

“Kila ninapofumba macho kuongea na Mungu Namuomba Akupe Maisha marefu na yenye baraka, Namuomba akupe Hekima busara na Ukue katika kumjua Mungu na  Kumheshimu Kila anayekuzunguka, Kuna wakati nazungukwa na matatizo nakaribia kukata tamaa lakini nikikufikiria wewe wewe tu Nanyanyuka na kufuta machozi na kupigana nayo ili nikulinde na Nihakikishe unaishi vyema na kujivunia kua na mama Kama Mimi”.

“Namshukuru sana Mungu kwa kukuleta kwangu Namshukuru Mungu kea kunipatia wewe ninahaidi kukutunza vyema na kuhakikisha hujutii kuwa na mama kama mimi , Amin I Love you Baby Dee”.

Hamisa alimalizia hivyo ujumbe wake kwa mtoto wake Prince Abdul Naseeb ‘Dylan’.

About this writer:

Diana

I am a hard working young woman Aspiring writer with dreams larger than life itself, always living by the principle that live today like there is no tomorrow.