Maua Sama Kufunga Ndoa Mwakani
Ndoa ni jambo la kheri sio kwa mwanamke tu, ila hata kwa wanaume, wasanii wengi wa Bongo wamekuwa hawadumu katika mahusiano na kuachana kila baada ya miezi michache,hii imefanya wasanii wengi washindwe kuingia katika ndoa , bado sababu haiko wazi lakini ni wasanii wachache wenye kukaa kwenye mahusiano kwa muda mrefu na kufikia hatua ya kufunga ndoa.
Mwanadada mrembo kabisa katika tasnia ya muziki wa Bongo fleva nchini, Maua Sama ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha” Katukatu’ amefunguka na kusema kuwa ndoa yake na mwanaume aliyemchumbia hivi karibuni inaweza kufanyika hapo mwakani lakini kwa sasa bado kidogo mipango ya harusi haijafanyika.Msanii huyo ambae miezi kadhaa hivi iliyopita alichumbiwa na mchumba wake mwenye asili ya kizungu anasema kuwa wanatarajia kufunga ndoa mwakani.
Maua Sama akiongea katika Over the Weekend ya gazeti la Ijumaa, alisema kuwa ana uhakika michongo yote ya harusi itaenda vizuri lakini kwa utaratibu wake na kazi zake kwa sasa hana mpango wa kufunga ndoa mwaka huu hadi mwakani.’Bado sana mipango ya ndoa kwa sasa mpaka mwakani.Sasa hivi ninaangalia zaidi muziki wangu,” aliongea Maua
Hata hivyo msanii Maua anasema kuwa anamshukuru sana Mungu maana ameweza kumsimamia na kuweka kukaa kwenye game muda mrefu huku nyimbo zake zikifanya vizuri ,lakini pia ameelezea sababu za msanii kukaa katika game la muziki kwa muda mrefu ni vile ambavyo msanii anaamua kujiweka “nashukuru nimeweza kukaa kwa muda mrefu bila kuchuja na hii ni kutokana na hii ni kutokana na msanii unavyojiweka” aliongezea Maua
Maua SaMa ambae pia ni zao zuri kutoka katika jumba la kulea wasanii wenye vipaji nchini la THT , amekuwa mmoja wa wanadada wanaofanya vizuri kuanzia katika wimbo wake wa ‘Mahaba niue’ ambao ulikaa muda mrefu kwenye chati, lakini hata baada ya wimbo huo nyimbo zilizofuata ziliendela kufanya vizuri na kupokelewa vizuri na mashabiki wake, akiwa pia ni mmoja wa wasanii wanaozunguka mikoani katika tamsha la Fiesta , maua amekuwa akipokelewa vizuri katika jukwaa la Fiesta.