Maneno Ya Diamond Baada Ya Kutoa Ngoma Mpya
Diamond Platinumz ni moja kati ya wasanii wakubwa ambao wamekuwa na roho ya kuthubutu kufanya kitu chochote ili mradi tu aweze kufanikiwa kimuziki, Diamond ambae tangu ameingia katika soko la muziki amekuwa ni mtu wa kufanya vizuri kwa kila ngoma anayoimba haijalishi ameshirikisha, ameshirikishwa au ameimba peke yake. Diamond ambae pia amekuwa mfano bora kwa baadhi ya wasanii na kujitolea kusaidia wasanii chipukizi wadogo na kuwakuza mpaka kujulikana Duniani kote anastaili kupewa pongezi kwa juhudi anazozionesha kila siku katika muziki na jinsi anavyoiwa vizuri Tanzania.
Ikiwa ni kama siku tatu tu zimepita tangu Diamond atoe wimbo wake mpya na kundi kubwa la muziki Duniani MorganHeritage unajulikana kama Hallelujah , msanii Diamond aliwakaribisha mashabiki wake kuangalia wimbo huo lakini aliwaambia pia mashabiki kile alichojifuunza baada ya kufanikiwa kutoa collabo hiyo.
Akiandika katika ukurasa wake wa Instagram Diamond aliandika'”#Hallelijah ft@morganheritage LINK IN MY BIO !(nyimbo hii ya #Hallelujah Imenifunza kwamba uwoga wetu na kutokujiamini unaotucheleweshea muziki wetu kuwa mkubwa Duniani,…pia umenifunza kuwa ukithubutu kila kitu kinawezekana ….Lakini pia imenifunza pia kuwa wana afrika mashariki tuna nafasi nzuri ya kuweza kuvuma duniani. Imenifunza pia kuwa hata ukiimba Kiingereza ila nyimbo ikiwa nzuri itapendwa na kuvuma kote hadi Uswahilini… Imenifunza pia mwenyezi mungu hana upendeleo ukijituma,ukawa na nia nzuri na ukimuomba atakuoa…..je wewe umejifunza nini)” haya ni maneno aliyoandika diamod huku pia akiwauliza mashabiki wake waweze kutoa maoni yao katika wimbo huo.
Wimbo wa Diamond na Morgan unaweza kuwa kithibitisho tosha kwa wasanii wengine kuwa kumbe kama una nia na unaweza kuthubutu basi unaweza kufanya vizuri, lakini pia Diamond amekuwa ni msanii anaejituma na kupambana sana ili kupata collabo kutoka nje ya nchi na akiaamini kuwa ili muziki wake ukue basi anawahitaji watu hao.diamond ametoa wimbo na wasanii wengi wakubwa duniani kama Ne-yo , P-square,.
Kama alivysema kutokuogopa kumemfanya aweze kusonga katika katika muziki, Diamond amekuwa kweli ni msanii mwenye kujaribu bila kuwa na uoga, nathanisasa ni muda wa wasanii wengi kuiga kile anachokifanya msanii Diamond.