Hemed Phd Akiri Kuwa Msanii Mwenye Watoto Wengi
Kuna tabia za wasanii hazibadiliki tena hasa Kwa wasanii wa kiume, wengi wamekuwa wakikataa kuwa na majukumu hasa ya kifamilia(watoto), kuwa na watoto sio jambo dogo , lakini pia sio jambo la mkosi, kuwa na mtoto ni jambo la kheri, kuna baadhi ya wasanii wakubwa tu nchini wamekuwa wakikata majukumu ya kulea watoto hao na kuwaachia wazazi wa upande wa pili kubaki wakiangaika na mizigo ya kulea peke yao.
Hemed Phd ambae kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘Mkimbie’ anasema kuwa amekuwa kimya kwa muda kwa sababu ya majukumu ya kifamilia”tunakuwa kimya kutokana na majukumu,majukumu ndio yanaweza kukubadilisha kutoka kwenye ujana kwenda kwenye ubaba, siwezi kusema kuwa ni mafanikio sana kwa sababu havikuja katika mipango kama nilivyotarajia,, hivi vitu vilihappen tu buubaa basi Mungu akafanya yake lakini ninajivunia kwa sababu ninaweza kuwahudumia watu ambao wananiangalia kwa kiasi kikubwa .Am proud to be a father'” alisema Hemed
Msanii Hemed Phd , alikiri kuwa hata yeye alikuwa akichomoa pale alipokuwa akiambiwa kuhusu taarifa za wanawake wake kumwambia wanaujauzito lakini inapokuja kwenye swala la mtoto anatoka amefanana nae kila kitu hivyo ni lazima akubali”kiukweli mwanzo nilikuwa nazingua kwa maana ya kwamba nilikuwa sizikubali mimba kabisa lakini copy zilivyotoka,wanangu wazuri sana,wanangu wamenizidi uzuri ivyo inabidid tu niwakubali maana wanafanana na mimi’ anaendelea kuongea
Hemed anasema kuwa hata hivyo , imekuwa tofauti kwa upande wake kwa sababu watoto wake wote hakuna ambae amebambikiziwa hata mmoja wote ni wa kwake na anawalea wote,kwa sababu hata matendo ya kupata mimba anavyofanya anakuwa anajua kipi kinafanyika.
Hata hivyo kwa muda sasa kumekuwa na tetesi kuwa pamoja na kuwa na watoto wengi lakini amekuwa akimpost mmoja tu” ni kweli ,lakini katika familia kuna mambo mengi, na bado ninayaweka sawa, yakikaa sawa ntawaweka wote , ila kwa sasa naomba ijulikana kuwa huyo ndo mwanangu na ifahamike ivyo kwa sasa” aliongezea Hemed
Kuhusu kuwa na watoto wengi hemed alipoulizwa ana watoto wangapi alijibu”ngoja nikatafute daftari langu kwanza niangalie idadi, ila nashukuru mungu tumeambiwa tuijaze Dunia kwaiyo kuwa na watoto wengi ni sawa tu’ aliongezea Hemed