Siwezi Kuamini Msiba wa Ruge Mpaka Nione Mwili Wake :-Mrisho Mpoto
Msanii mkongwe wa nyimbo za asili nchini Mrisho Mpoto amefunguka alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika msiba wa Ruge Mutahaba uliopo nyumbani kwa wazazi wake huku jijini Dar huko mikocheni .
Akiongea na waandishi wa habari Mrisho Mpoto anasema kuwa hakuna msanii mkubwa anaeonekana kwa sasa anaendesha gari na nyumb nzuri bila kupita mikononi kwa Ruge hata mmoja , hayupo Tanzania.
Hata hivyo Mrisho Mpoto anasema kuwa kamwe hawezi kukaa na kuamini kuwa Ruge amekufa mpaka pale atakapoona katika jeneza mwili wa Ruge ambae kwake ni kama kaka aliemshika mkono kumfanya ainuke.
Wasanii ni wengi sana na watu wa nyanja mbalimbali ambao wamekuwa wakitoa ushuhuda wa kile ambacho walifanyiwa na jasiri kiongozi huyo ambae mshumama wake umezima ghafla.