Nawapenda Wanawake Waliokaza,Sio Wema -Rado
Msanii wa maigizo nchi ambae pia alishawahi kujaribu upande wa muziki na akafanya vizuri anaejulikana kama Rado, amefunguka na kusema sifa za mwanamke anaempenda lakini amekanusha kabisa kuwa yeye hawezi kutembea na mwanamke anaetoka Bongo Movie au Bongo Fleva.Msanii huyo ambae alikuwa akiongea na waandishi wa habari na kuulizwa kuhusu kazi yake iliyo toka kipindi cha nyuma kidogo , filamu ambayo alicheza na Tanzanian Sweetheart Wema Sepetu iliyojulikana kwa jina la “Madame’ ambayo pia ilizua maneno na tetesi za msanii huyo wa kiume kutoka kimapenzi na Wema Sepetu, Rado alifunguka na kusema hawezi kutembea na Wema hata kidogo.
‘Sijawahi kumpenda msanii yeyote wa Bongo Movies au wa Bongo Fleva wa kike na siajwahi tu kuvutiwa nao hata kidogo, sijawahi kuvutiwa na Madame Wema Sepetu kwa sababu naona yupo nje ya wanawake ninao wapenda” alifunguka rado, lakini pia msanii huyo wa alitoa sababu za yeye kutokuvutiwa kimapenzi na msanii wa kike akiwemo madame Wema Sepetu au wanawake wote kutoka Bongo Movie na Bongo Fleva na kusema kuwa “unajua mimi ni mchanganyiko wa Usukuma na Unyakyusa, kwaiyo wanawake wa kudeka muda wote siwapendi, napenda wanawake fulani hivi waliokaza” ameongezea Rado
Akielezea experience aliyoipata kutoka kwa Madame Wema wakiwa katika kuigiza filamu ya ‘madame’ , Rado anasema kuwa Wema Sepetu anaonekana mwanamke wa kudeka sana kwaiyo mtu kama huyo hawatawezana kwabisa,” kwa jinsi alivyokuwa mlegevu Madame, sina hata uhakika hata kama anaweza kufua , kutokana na kudeka kwake” anaendelea Rado
kwa upande wa Bongo Movies, Rado anasema kuwa kwa sasa tasnia ya filamu inaendelea kufanya vizuri kutokana na jitihada zinazofanyika ili kulinda vipaji vya wasanii ambapo kumekuwa na kampeni mbalimbali ikiwemo ile ya kusimamisha uuzaji wa filamu fake mitaani na anasema kwa sasa vilio wa wasanii wa filani vinaelekea kuisha na wataanza kuona maslahi ya kazi wanazofanya na kuna baadhi ya makampuni yamejitolea ilii kusimamia kazi za wasanii katika uuzaji.