Free Talk Show Kipindi Kinachowatolea Uvivu Wasanii
Si kawaida kwa watu kukosoa pale wanapoona kuna kitu kimekosewa , na mara nyingi ni kwa sababu wengi wetu tunaongopa kutengeneza uadui na wale watu ambao wamekosea.Labda kwa sababau wengi hawaonekani kuwa wabaya au hawataki kuwa maadui kwa watu wao wa karibu.katika tasnia ya muziki sio hapa Tanzania tu bali hata nje ya Tanzania kuna baadhi ya vitu wasanii wanafanya ambavyo labda kwa namna moja ama nyingine mashabiki hawaoni au wanaona lakini hawana pa kusemea, lakini pia labda wapo wanaoona lakini inakuwa vigumu kusema moja kwa moja kwa mhusika.
Free Talk Show ni kipindi cha televisheni kilichaanzishwa hivi karibuni na vijana wa bongo wakiwa na lengo la kurekebisha mambo madogomadogo ambayo yamekuwa yakitokea kwa msanii binafsi au kwa kazi yake anayoifanya kwa ujumla,lengo ikiwa si kumfanya yule anaekosolewa au kusifiwa aonekane bora kuliko mwingine hapana lakini pale ukweli unapotolewa ndio unaomfanya mtu ajirekebisha na anaposifiwa basi anaongeza bidii.
Kipindi cha nyuma kulikuwa na mwanadada Salam Jabir ambae alijitolea kwa moyo wote kukosea na kusifia wasanii pale wanapopatia au kukosea, lakini baada yake kumekuwa kimya wasanii hawakosolewi tena kama zamani.
Kipindi hicho ambacho kinaonyeshwa katika televisheni ya channel E nchini Tanzania siku ya Jumatano na kurudi wa siku ya Jumapili mchana na Jumatatu mchana kimekuwa chachu kwa sababu kimekuwa kikiwakosoa wasanii bila kuogopa umaarufu au ukubwa wa msanii fulani.Kuna baadhi ya video za wasanii zimekuwa zikirudiwa au kuigwa kutoka nchi nyingine lakini watu wamekuwa wakinyamzia hayo.
Kikiongozwa na Alice Kella ambae yeye pia ni mmoja wa wasanii wa bongo fleva inaonekana ameshaona madudu yanayofanyika kwa wasanii wenzake, akiwa pamoja na Victor Mgonja na Susan J Odere maarufu kama Taiya Odere wamekuwa manaodha wazuri na endapo wataendelea hivyo basi lengo la kukuza muziki wa Tanzania litakuwa linakaribia kufanikiwa kwa kiasi chake.Ingawa wapo baaadhi ya mshabiki wameanza kuwashambulia waandaaji wa kipindi icho lakini nadhani hizi ndizo njia sahihi za kukuza muziki.