Ndoa Ya Juma Kapuya na Binti Wa Miaka 25 Yazua Gumzo
Ndoa ya aliyewahi kuwa Mbunge wa Urambo mkoani Tabora, miaka ya nyuma Juma Kapuya mwenye umri wa miaka 74 na binti wa miaka 25 ambayo ilifungwa siku ya jumapili imezua gumzo kubwa katika Mitandao ya kijamii.
Picha na video kadhaa zilizosambaa kwenye Mitandao ya kijamii zimemuonyesha Profesa Juma Kapuya ambaye ni mtu mzima kupitiliza akimuoa binti huyo mdogo ambaye anaweza akawa binti yake aliyeatambulika kama Mwajuma Mwiniko na ndoa ilifungwa wilayani Urambo, mkoani Tabora.
Profesa Juma Kapuya alikuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kuanzia mwaka 1997 hadi 2005 na baadaye akateuliwa na Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Waziri wa Ulinzi (mwaka 2006) na kisha kuwa Waziri wa Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo nafasi aliyoteuliwa mwaka 2008.