Mange Kimambi Amlilia Diamond Amsamehe Baba Yake
Mange Kimambi amemuandikia ujumbe wa wazi staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz kuhusu kumsaidia baba yake mzazi Mzee Abdul Juma ambaye anatajwa kuwa mgonjwa.
Kwa muda mrefu kumekuwa na Ugomvi wa kifamilia kati ya Diamond na baba yake ambapo amewahi kuweka wazi kuwa hajalelewa na baba yake bali na Mama yake ambaye ndiye anayemjali.
Wiki iliyopita Baba yake na Diamond aliweka wazi kuwa anaumwa na anasumbuliwa na maradhi mbali mbali ikiwemo miguu ambayo ipo katika hali mbaya na kumlilia mwanaye amsaidie japo akapate matibabu.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mange amemuomba Diamond aweke tofauti zao pembeni na amsaidie baba yake ambaye yupo katika hali mbaya:
https://www.instagram.com/p/Bt-nyKVBEgD/?utm_source=ig_share_sheet&igshid=tevtyrdp2c9w