Penzi la Sista Fey na Kibenten Chake Ladaiwa Kufika Mwisho
Msanii wa Bongo movie Faidha Omary maarufu kama Sista Fey amedaiwa kuachana na mume wake ambaye anatajwa kuwa na umri mdogo kuliko yeye (kibenteni) baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa miezi kadhaa.
Sista Fey na mpenzi wake Hollystar walijipatia umaarufu kwenye mitandao ya kijamii mwaka jana baada ya video zao wakifanya vituko mbali mbali kuangaliwa na watu wengi.
Lakini siku chache zilizopita kuna tetesi zilisambaa kwamba wawili hao hawapo pamoja baada ya kila mmoja kufuta picha za mwenzake kwenye mitandao ya kijamii na hata kila mm0ja kuacha kumfollow mwenzake,
Kwenye mahojiano aliyofanya na Global Publishers, Sista Fey bamekataa tetesi za kuachana na mume wake huyo ambaye alifunga naye ndoa miezi michache iliyopita;
Jamani hatujaachana ni kwamba pale tulipokuwa tunaishi tumehama, tumehamia sehemu nyingine halafu kuhusu hizo picha zangu kufutwa mtandaoni, nilichukua simu yake nikazifuta picha zangu na kwenye simu yangu nikafuta zake,
Tumefanya hivyo kwa sababu sasa hivi nimeamua kufanya kazi za kijamii maana mambo ya mapenzi hatuhitaji tena kuyaweka mtandaoni, ila kwa sasa sijapata usajili wangu ndio maana nipo nafanya kazi na Flora Nitetee kwa ajili ya kusaidia jamii.”