Familia Yafungukia Kifo Cha Godzilla na Ratiba Ya Mazishi
Familia ya aliyekuwa Msanii wa hip hop nchini Godzilla wamefunguka na kuweka wazi ratiba ya mazishi mara Baada ya kufariki siku ya jana.
Baba mdogo wa mwanamuziki huyo amesema ndugu yake aliteswa na kitu kilichokwama tumboni kwa zaidi ya siku tatu na kumfanya atapike mfululizo.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5, Joyce amesema mwanamuziki huyo Golden Mbunda alikuwa akitapika kwa siku tatu mfululizo.
Jumapili (Februari 10, 2019) alilala muda mrefu, haikuwa kawaida. Baadaye akaomba barafu tulivyompa akaanza kutapika ndipo tulipompeleka hospitali na kugundulika ana malaria, sukari imepanda sana na presha imeshuka.
Pia marehemu alisema kuna kitu kiling’ang’ania tumboni kama vile kinataka kutoka ila kinagoma, alijaribu kukitoa kwa kujitapisha lakini hakikutoka“.