Stara Thomas-Wasanii Wengi Mavazi Yao Hayana Stara
Msanii mkongwe wa muziki wa Bongo fleva Mwanamama Stara Thomas amewaibukia wasanii wakileo na kuyachambua mavazi yao na kusema hayana Stara wala heshima.
Stara alifunguka hayo kwenye mahojiano aliyofanya na mtandao wa Dizzim Online na kuweka wazi kuwa hicho ni moja kati ya vitu ambavyo vinamkera kwenye Sanaa ya Leo ni wasanii kukosa maadili.
Maadili Kama maadili nikijaribu kuyaangalia kwa vijana ambao kwa sasa hivi wanafanya muziki wanajisahau sana, mavazi yao hayana Stara kwani wasanii wengi Hivi sasa wana mentality moja kwamba eti ‘Tunaenda na fashion’”.